SHUKURANI
Kwanza, namshukuru sana Mungu kwa ajili ya ukuu na uweza wake ambao nimeuona katika kipindi chote cha maisha yangu; hususani katika kipindi cha kuandika tasnifu hii, ambapo nimekutana na changamoto nyingi, lakini kwa upendo wa Mungu niliweza kusonga mbele. Pili, kwa namna ya pekee namshukuru sana msimamizi wangu, Prof. J.S. Madumulla. Ameniongoza vizuri na kuniimarisha sana katika uandishi wa tasnifu. Ustahimilivu, mwongozo na upendo aliouonyesha kwangu ni mkubwa. Namwomba Mungu ambariki sana. Tatu, ninawashukuru sana walimu wangu walionifundisha masomo yangu katika ngazi hii ya Uzamili ambao ni Prof. J.S. Madumulla, Dkt. Elias Manandi Songoyi, Dkt. Rafiki, Dkt. Seif Khatibu, na Dkt. Athumani Ponera. Nimejifunza mambo mengi sana kutoka kwao, ambayo yamekuwa na mchango mkubwa wa kuniwezesha kufikia hapa nilipo. Mungu awabariki sana. Pia, nawashukuru sana walimu wangu walionifundisha tangu shule ya msingi hadi shahada yangu ya kwanza. Pia wanafunzi wenzangu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii. Nne, nawashukuru sana wazazi wangu, kwani wamekuwa na mchango mkubwa sana wa kuniwezesha kufika hapa nilipo. Mungu awabariki sana na awajalie maisha mazuri na marefu. Tano, namshukuru sana mume wangu mpenzi ambaye amenipa ushirikiano mkubwa wa kipesa na kimawazo katika kuniwezesha kukamilisha masomo yangu. Pia, ninamshukuru kwa uvumilivu mkubwa ambao ameuonyesha katika kipindi chote ambacho nilikuwa katika masomo yangu. Mungu ambariki sana. Na mwisho, ninawashukuru sana watoto wangu, Gladness Lusungu Kibangali, Glory Lusungu Kibangali na Graciosness Lusungu Kibangali, kwa uvumilivu waliouonyesha v katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikishughulika na masomo yangu. Mungu awabariki sana.