SHUKRANI
Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia nguvu, uzima, afya njema na kuniwezesha kuifikisha kazi hii katika hatua hii. Pili, shukrani zangu za pekee zimwendee msimamizi wangu, Dkt. Muhammed Seif Khatib, ambaye amekuwa nami bega kwa bega katika kunishauri, kunikosoa, kutoa mwongozo na mapendekezo ili kuhakikisha kazi hii inafanyika na kukamilika. Asante sana na Mungu akubariki. Aidha, nawashukuru wahadhiri wangu Dkt. Athuman Ponera, Dkt. Rafiki Sebonde na Dkt. Zuhura Badru kwa kuniimarisha kitaaluma. Tatu, shukrani zangu za dhati nazifikisha kwa wazazi wangu wapendwa, marehemu baba yangu Taufiq Zungiza na mama yangu Wakti Zaid kwa uvumilivu wao katika hatua zote za makuzi niliyopitia. Hawakuchoka katika kila hatua bali walipambana ili nifike hapa nilipo leo. Pia, sitaiacha familia yangu ambayo ilinipa moyo na kunitia nguvu katika kipindi chote cha masomo na kuandaa kazi hii. Miongoni mwao ni dada yangu kipenzi Mwatum Taufiq pamoja na Zafarani Taufiq, Burton Mwemba, Hussein Zaid bila kuwasahau Whitney, Queen, Hawa na Aqbar. Wote hao walijitoa bila kuchoka kwa kunipa muda mzuri wa kujisomea, kunipa ushauri pale nilipochoka na kuniombea. Asanteni nyote, Mungu awabariki. Nne, nawashukuru wanafunzi wenzangu wa Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili. Miongoni mwa wengi ni pamoja naKuruthum Mazongela, Haruwa Mohammed,Martina Duwe na Denis Ponera kwa michango yao mizuri na ushauri wenye manufaa. Aidha, sitawasahau Bw. na Bi Fred wa Tanga mjini kwa ukarimu na kujitoa kwao kuhakikisha kazi hii inakamilika. Pia, napenda kuishukuru familia ya Mwinyihatibu kwa kunipa ushirikiano katika kipindi chote cha kukusanya data nilipokuwa Tanga kwa ajili ya utafiti huu.